Kampuni ya Sportpesa Ndio Wadhamini wa Makala ya Mashindano ya Chipukizi

Makala ya kwanza ya mashindano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka ishirini baina ya chipukizi wa timu za ligi kuu ya Sportpesa yatakayoanza tahere 17 hadi 30 mwezi ujao, yamepata udhamini kutoka Sportpesa. Kulingana na afisa mkuu wa kampuni ya Sportpesa, Ronald Karuri, makala matatu ya mashindano hayo yatapokeaA� udhamini wa shilingi milioni 6.2 huku mashindano hayo yakiandaliwa wakati wa likizo za shule ili kuwapa wanafunzi fursa ya kushiriki.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, Karuri alisema kuwa, lengo kuu la mashindano hayo ni kuunga mkono juhudi za kuboresha soka katika maeneo ya mashinani na akatoa wito kwa mashirika mengine kuunga mkono juhudi hizo.

Mshindi wa mashindano hayo atatia kibindoni shilingi laki tano.