Kampuni ya SONY yapanga kuanzisha ukuzaji wa miwa

Kampuni ya sukari ya South Nyanza A�(SONY) inapanga kuanzisha ukuzaji wa miwa inayokomaa haraka ili kukabiliana na uhaba wa mara kwa mara wa miwa. Kaimu mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo A� Bernard Otieno amesema uhaba wa miwa wanaoshuhudia unasababishwa na ongezeko la A� visa vya unyakuzi wa miwa unaotekelezwa na kampuni jirani za sukari . Amesema wakuzaji wengi wa miwa waliokuwa wakikuza miwa kwa wingi wameanza kukuza vyakula. Wakati huo huo amesema hawatapunguza bei za miwa na sukari ili kuimarisha faida yao. Otieno amesema wanakabiliwa na wakati mgumu katika kutafutia masoko sukari yao kutokana na hali ya sukari ya bei nafuu inayaoagizwa kutoka nje jambo ambalo limelazimu kampuni za sukari kupunguza bei zao. Kulingana na Otieno hatua ya kupunguza bei za sukari itasababisha hasara kubwa kwa sababu gharama ya uzalishaji ingali juu.