Kampeni Ya Kuangamiza Tohara Ya Wasichana Yaanzishwa Narok

Zaidi ya wasichana-200 duniani ni waathiriwa wa upashaji tohara licha ya harakati zinazoendelea za kukabiliana na uovu huo. Akiongea katika kituo cha wasichana cha Tasaru, mkurugenzi wa kimataifa wa usawa Sheilby Quast alisema wamezindua kampeni ya kuangamiza mila hiyo katika kaunti ya Narok. Alisema wana hofu kwamba wasichana wengi wangali wanaozwa wakiwa na umri mdogo baada ya kupashwa tohara. Alisema tayari umoja wa mataifa umezindua mipango ya kukomesha uovu huo duniani. Mkurugenzi wa kituo cha Tasaru, Agnes Paraiyo alisema watachunguza jinsi shughuli ya upashaji tohara inavyotekelezwa siku hizi na vile vile kukabiliana na ndoa za mapema katika kaunti ya Narok. Msimamizi wa maswala ya watoto katika kaunti ndogo ya Narok, Julius Ngoko alisema ipo haja ya juhudi za pamoja ili kuangamiza kabisa uovu huo katika kaunti hiyo. A�