Kampeini ya kitaifa ya a�?Boresha Machoa�? yafanya upasuaji wa macho

Wiki moja baada Mama wa taifa. Bi. Margaret Kenyatta kuzindua kampeini ya kitaifa ya a�?Boresha Machoa�?, kundi la kwanza la walengwa wa mradi huo lilifanyiwa upasuaji wa macho kwenye hospital moja Jijini Nairobi. Kampeini ya kitaifa ya a�?Boresha Machoa�?, ni ushirikiano kati ya mradi wa Mama wa taifa wa a�?Beyond Zeroa�? na mipango ya a�?Ahadi Kenyaa�?, a�?Vision Springsa�? na Hospitali ya macho ya Nairobi (UHEAL). Ma-elfu ya WaKenya walio na shida za macho wanatarajiwa kufaidika na mradi huo, uliozinduliwa Jumatano iliyopita katika kituo cha Bura, ambako alikutana na ma-elfu ya kina mamaA� na viongozi wao kutoka pembe zote za Kaunti ya Taita Taveta. Wakati wa mkutano wa hadhara ulio-andaliwa na shirika laA� Maendeleo Ya Wanawake -(MYWO), katika kituo hicho cha Bura, wakaazi kadha walio na shida za macho katikaA� kaunti ya Taita Taveta, walifanyiwa uchunguzi, ambapo kundi la kwanza la wagonjwa lilitambuliwa na maafisa wa mradi wa UHEAL naA� Vision Springs.A� Mmoja wa wagonjwa hao alisema ameishi na tatizo la mboni za macho tangu mwaka 1998. Mtaalamu mmoja wa kimatibabu kutoka chuo kikuu cha Nairobi, alisema matatizo ya mboni za macho ni miongoni mwa yale yanayosababisha upofu sio tu nchini Kenya, bali duniani kote.