Kamishna Tororey wa IEBC amestaafu

Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC, Praxedes Tororey amestaafu. Tororey amestaafu baada ya kutimiza umri wa miaka 60. Alikuwa miongoni mwa maafisa ambao muungano wa NASA umekuwa ukishinikiza waondolewe kwa madai ya kuvuruga uchaguzi mkuu tarehe 8 mwezi Agosti. Maafisa wengine kwenye orodha ya NASA ambao wametakiwa kuondoka kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais ni pamoja na makamishna Abdi Guliye na Boyu Molu, afisa mkuu wa tume ya IEBC, Ezra Chiloba, mshauri wake Moses Kipkosgey na mkurugenzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano James Muhati. Uamuzi wa kina wa mahakama ya juu uliosomwa siku ya Jumatano haukuwahusisha maafisa wowote katika madai ya kuborongwa kwa uchaguzi mkuu.