PAC Yahoji Kampuni Ya Murkomen Kuhusiana Na NYS

Kamati ya Bunge ya uhasibu wa pesa za (PAC) imeihoji kampuni ya seneta wa Elgeyo Marakwet kipchumba Murkomen kuhusiana na madai ya kuhusika katika sakata ya shirika la huduma ya vijana kwa taifa NYS. Akiwa mbele ya kamati hiyo msimamizi na mshirika wa kampuni hiyo Hillary Kiprotich Sigei alikiri kwamba kampuni ya mawakili ya Singa��oei Murkomen na Sigei ilipokea kutoka kwa kampuni ya Out of the Box Solutions iliyolipwa kutoka kwa akaunti za NYS kwa huduma za kitaalamu ilizotoa. Segei alisema kampuni ya Out of Box Solutions ililipa kampuni yao shilingi milioni 15, milioni 8 kupitia akaunti ya benki ya Co-operative na milioni 7 kupitia akaunti ya Family Bank. Hata hivyo Sigei alisema kwamba kampuni yao haikupokea pesa kutoka kwa mtu yeyote ama kampuni iliyotajwa sana katika sakata ya NYS.