Kamati Ya Bunge Nchini Brazil Yaidhinisha Pendekezo La Kumuondoa Rais Dilma Rousseff Mamlakani

Kamati ya bunge nchini Brazil imeidhinisha pendekezo la kumuondoa mamlakani Rais Dilma Rousseff, anayekabiliwa na mashtaka ya kukiuka kanuni za utayarishaji bajeti ili kufanikisha kuchaguliwa kwake tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2014.

Baada ya mjadala mkali, kamati hiyo ilipiga kura kwa asilimia 38 kwa 27 na kupitisha kuondolewa kwake madarakani.Bunge la waakilishi nchini humo sasa linatarajiwa kupigia kura pendekezo hilo siku ya jumapili.

Thuluthi mbili ya wabunge kwenye bunge hilo wakipitisha hoja hiyo,itawasilisha kwa bunge la seneti,ambapo ikipitishwa na wabunge rais huyo atasimamishwa kazi kwa miezi sita huku bunge la seneti likijadili hatma yake.Katika kipindi hicho naibu rais Michel Temer atahudumu kama kaimu rais.

Mnamo mwaka 1992 aliyekuwa rais wa nchi hiyo Fernando Collor de Mello alijizulu kabla ya bunge la seneti kujadili hoja ya kumuondoa mamlakani kufwatia madai ya ufisadi dhidi yake.

Rais Rossef hata hivyo amekana madai ya kuvuruga akaunti za serikali akitaja madai hayo kuwaA� mapinduzi ya kisiasa.