Kamati Teule Ya Bunge Yahairisha Vikao Kufuatia Kauli Ya IEBC

Kamati teule ya pamoja ya mabunge yote mawili inayochunguza mfumo wa uchaguzi hapa nchini imeahirisha vikao vyake hadi saa tisa alasiri baada ya makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka wakiongozwa na mwenyekitiA�A�Isaack Hassan kuhoji mamlaka ya kamati hiyo. Makamishna wa tume ya IEBC ambao walikuwa mbele ya kamati hiyo leo asubuhi walilaumu wabunge kwa kukiuka kifungu cha 251 cha katiba ambacho kinaratibu njia ya pekee ya kuwaondoa makamishna hao. Hassan alisema haki zao zinakiukwa. Makamishna hao walikuwa wameagizwa kufikaA�mbele ya kamati hiyo pamoja na maafisa wa makao makauu ya tume hiyo kujibu madai ya utovu wa maadili. Kamati hiyo inayongozwa na wenyevit wenza James Orengo na Kiraitu Murungi.