Kamanda Wa Polisi Siaya Atetea Hatua Ya Maafisa Wa Polisi Kufyatua Risasi Wakati Wa Maandamano

Kamanda wa polisi katika kaunti ya A�Siaya Chrispus Mutali ametetea hatua ya maafisa wa polisi ya kufyatua risasi wakati wa maandamano ya A�upinzani dhidi ya tume ya IEBC mjini Siaya siku ya jumatatu, akisema walifanya hivyo kwa usalama wao.Hii inafuatia ripoti kwamba maafisa 29 wa polisi huko Siaya walijeruhiwa wakati wa maandamano hayo, ambapo watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.Maafisa hao walisafirishwa kwa ndege hadi jijini Nairobi kwa matibabu maalum.Akiongea na wanahabari A�mjini Siaya, kamanda huyo wa polisi wa utawala alisema polisi walilazimika kufyetua risasi baada ya waandamanaji hao kumkamata afisa mmoja wa polisi na kuanza kumnyonga huku wengine wakijaribu kuvunja lango la afisi za tume ya IEBC za Siaya.Mutali alisema matumizi ya vitoza machozi na risasi za mpira hayakuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wakiwashambulia polisi kwa mawe, vijiti na Kombeo.Mutali alisema polisi hawakuwa na jingine na kufanya ila tu kufyetua risasi ili kuwaokoa wenzao na wao wenyewe.Amekanusha madai kwamba waandamanaji hao hawakuzusha fujo zozote akisema wao ndio walianza kuwashambulia polisi kwa mawe.Waandamanaji wengine sita wamelazwa katika hospitali kuu ya Siaya na wengine kuhamishwa hadi hospitali ya Moi Teaching and referral huko Eldoret na ya Jaramogi Oginga Odinga jijini Kisumu.