Kalonzo na Wetangula Wawarai Wakazi Wa Meru Kujisajili Kwa Wingi

Vinara wenza wa muungano wa CORD Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula walipeleka kampeni zao za kuwahamasisha watu kujisajili kuwa wapiga kura katika kaunti ya Embu ambako waliwahimiza wakazi wa eneo la mlima Kenya kujiunga na muungano wa NASA. Musyoka alisema itimiapo wakati wa uchaguzi mkuu tarehe 8 mwezi Agosti, nchi hii itakuwa na mwanzo mpya utakaokuwa na marekebisho mengi na wakazi wa eneo la mlima Kenya wapasa kushiriki katika kuleta marekebisho hapa nchini. Akiongea baada ya kufungua ofisi ya chama cha Wiper mjini Embu, Musyoka alisema nchi hii sasa inakumbwa na migawanyiko zaidi na akataja changamoto zinazowakumba wakenya chini ya serikali ya Jubilee Maoni sawa na hayo yalitolewa na kinara mwenza Moses Wetangula ambaye alisema muungano wa NASA ndio suluhu la pekee ka kuangamiza ufisadi, ikabila na umaskini ambavyo vimekithiri kwenye serikali ya jubilee. Aliwahimiza Wakenya kujiepusha na ukabila.