Kalonzo ashtaki serikali kwa kuondoa walinzi, bastola

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amewasilisha kesi mahakamaniA�A�kulalamikia uamuzi wa serikali wa kuondoa walinzi wake na bastola yake. Kwenye kesiA�A�ya dharura, kiongozi huyo wa chama cha Wiper alitaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria.Sasa anaitaka mahakama kutoa agizo la kuwazuiaA�A�polisi kuingilia matumizi ya bastola yake ya Beretta ambayo amekuwa nayo tangu mwaka 1998. Mahakama kuu jijini Nairobi siku ya jumanne ilitoa maagizo ya muda ya kurejeshwa kwa walinzi wa wabunge 141 wa NASA waliondolewa baada ya uapisho wa kiongozi wa mrengo huo Raila Odinga .JajiA�Roselyne Aburili aliagiza pande hizo mbili kufika mahakamani katika muda wa wiki mbili zijazo kwa kesi hiyo . Kupitia wakili wao Peter Kaluma, walisema kuondolewa kwa walinzi wao kunahatarisha maisha yao.