Kalonzo amewahimizi wakazi wa Nyamira kujisajili ili kuiondoa Jubilee mamlakani

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amewahimiza wakazi wa kaunti ya Nyamira wajisajili kwa wingi kuwa wapiga kura ili kuiondoa mamlakani serikali ya jubilee wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Akiongea katika eneo bunge la Borabu, Musyoka aliishutumu serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kwa kutotekeleza majukumu yake ipasavyo hasa katika vita dhidi yaA� kundi la wapiganaji la Al ShabaabA� nchini Somalia ambalo limewaua wanajeshi kadhaa wa Kenya miezi ya hivi majuzi. Alisema yeye ndiye anayefaa zaidi kuchaguliwa kuwa rais kwa sababu ana ujuzi mwingi katika masuala ya diplomasia nchini na kimataifa. Mbunge wa Borabu Ben Momanyi alitoa wito kwa wakazi wa sehemu hiyo kumuunga mkono Musyoka , akisema wakati mmoja alikuwa makamu wa Rais na ana ujuzi wa kutosha wa kuiongoza nchi hii.Mgombezi wa eneo bunge la Mugirango magharibi Stephen Mogaka aliishutumu serikali ya jubilee kwa kutoa ahadi za uongo za ujenzi wa miundo msingi hasa barabara huko Nyamira