Kalonzo ajizatiti kupata tiketi ya kuwania urais ya NASA

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka sasa anasema atajizatiti kupata tiketi ya kuwania urais ya muungano wa NASA na wale wanaomsubiri anga��atuke wamepotoka. Kalonzo ambaye alisema udhaifu wake mkubwa umekuwa kuwaamini watu wengine, aliwalaumu washindani wake ndani na nje ya NASA kwa kumtaja kuwa kugeugeu. Akiongea katika ukumbi wa Bomas of Kenya wakati wa mkutano na wawaniaji nyadhifa mbali mbali wa chama hicho, Kalonzo aliwapuuzilia mbali wahakiki wake kuhusu uamuzi wake wa kutaka kuwania urais akisema ametosha kuwania wadhifa huo. Kiongozi huyo wa Wiper hata hivyo alisema atawaonyesha wahakiki wake maadili yake halisi ya kisiasa.Matamshi haya yake yalikaririwa na viongozi wa chama hicho, ambao waliwalaumu washindani wake ndani na nje ya NASA kwa kueneza dhana kwamba Kalonzo sio mtu wa kuaminika. Karibu sarakasi zizuke kwenye mkutano huo baada ya gavana wa Kitui Julius Malombe kumlaumu mpinzani wake kwenye uwianiaji kiti cha gavana David Musila kwa kupanga kutumia ushawishi wake kushinda uteuzi wa chama hicho tarehe 4 mwezi ujao.