Khalifa Sanogo ndiye mgombeaji wa kwanza kujitosa katika kinyanga��anyiro cha urais, Mali

Meya wa mji wa Sikasso nchini Mali ndiye mgombeaji wa kwanza kujitosa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa urais mwaka-2018. Khalifa Sanogo ambaye alikuwa muuzaji majora kabla ya kuingia kwenye siasa amesema atawania kiti hicho kwa tikiti ya chama cha Alliance for Democracy in Mali-ADEMA ingawa lazima aibuke mshindi kwenye mchujo wa chama hicho. Tangazo lake limewashangaza wafuasi wa rais Ibrahim Boubacar Keita kwani chama cha ADEMA kinaunga mkono chama cha Rally For Mali kinachoongozwa na rais Keita katika bunge la nchi hiyo na hakikutarajiwa kuwa na mgombeaji urais. Keita hajatangaza ikiwa atawania hatamu ya pili ingawa huenda akatangaza azma hiyo baada ya kukamilika kwa hatamu yake.