Kaka wa Kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong afariki kutokana na shambulizi za kemikali

Kaka wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong a��UnA� aliuawaA� kutokana na shambulizi la kemikaliA� nchini Malaysia kufwatia amri ya serikali ya taifa hilo, kulingana na duru za kijasusi za Marekani.

Kim Jong-nam alifariki dunia katika mazingira tatanishi kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur,huko Malaysia mnamo mwaka wa 2017,wakati wanawake wawili walipompaka usoni kemikali inayoathiri mishipa ya neva.Marekani imesema kuwa kufwatia ugunduzi huo ,itaiwekea Korea kaskazini vikwazo vya kichumi.Marekani mara kwa mara imeshutumu sera za Korea kaskazini.