Kaimenyi amtetea Matianga��I na kukashifu upizani

Waziri wa ardhi Jacob Kaimenyi ametoa wito kwa upinzani kutoingilia mipango ya usalama inayotekelezwa na serikali kwa lengo la kuwezesha kuandaliwa kwa uchaguzi wa amani.Akiongea mjini Meru,Kaimenyi alisema sio haki kwa upinzani kudai kwamba kaimu waziri usalama wa taifa Dakta Fred Matianga��i anatumiwa na serikali ya Jubilee kuzua hofu miongoni mwa Wakenya ili wasijitokeza kupiga kura.Kaimenyi alisema hatua zinazochukuliwa na waziri Matianga��I pamoja na inspekta jenerali wa polisiA� zinalenga kuhakikisha kuwa kuna usalama kote nchini wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu ujao na wala sio kuwatisha wapiga kura kama inavyodaiwa na upinzani.