Kabras Sugar inanuia kufuzu katika mashindano na ‘Dala Seven’

Kabras Sugar itanuia kufuzu kwa fainali ya mashindano ya raga ya ‘Dala Seven’, ambayo ni ya mwisho kwenye msururu wa taifa, kunyakua ubingwa wa msururu huo wa raga kwa wachezaji saba kila upande.

Kabras ilitetea taji ya mkondo wa ‘Christie’ baada ya kuishinda Impala alama 19 kwa 7 mwishoni mwa juma jijini Nairobi. Huku Homeboyz na Impala pia zikiwa na nafasi ya kutwaa ubingwa wa taifa, Kabras italazimika kuandikisha matokeo bora kundini ‘A’ dhidi ya Oilers, Nondies na MMUST. Impala na Homeboyz zinazowania taji hiyo msimu huu, zimetengwa kundini ‘B’ pamoja na Bulls na Kisii huku kundi ‘C’ ikishirikisha Nakuru, KCB, Blad na Kisumu. Kundi ‘D’ linazijumwisha Quins, Mwamba, Strathmore na Makueni. Baada ya mikondo mitano ya mwanzo, Kabras inaongoza msururu huo kwa alama 85; tano mbele ya Impala nayo Homeboyz ni ya tatu kwa alama 78.