Justin Muturi na Ken Lusaka wapendekezwa kuwa maspika

Chama cha Jubilee kinachoongozwa na rais Uhuru Kenyatta kimekubaliana kwa kauli moja kumpendekeza Justin Muturi kuwa spika wa bunge la taifa na aliyekuwa gavana wa Bungoma Ken Lusaka kuwa spika wa Senate. Naibu wa Muturi amependekezwa kuwa mbunge wa Kuresoi kaskazini Moses Cheboi naye Kithure Kindiki amependekezwa kuwa naibu spika wa Senate. Chama chaA� Jubilee pia kilikubaliana kwamba mbunge wa Garissa mjini Adan Duale atakuwa kiongozi wa wengi bungeni naye seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kuwa kiongozi wa wengi katika senate. Naibu wa Duale atakuwa mbunge wa Kitutu Chache kaskazini Jimmy Angwenyi huku naibu wa Murkomen akiwa seneta wa Isiolo Fatuma Dulo. Mbunge wa Mumias mashariki Benjamin Jomo Washiali aliidhinishwa kuwa kiranja wa bunge la taifa ambapo naibu wake atakuwa aliyekuwa mbunge wa Runyenjes Cecily Mbarire.A�Wengine ni seneta wa Nakuru Susan Kihika aliyependekezwa kuwa kiranja wa senate na naibu wake akiwa seneta wa Murang’a Irungu Kanga��ata. Rais Kenyatta alikutana na wabunge waliochaguliwa kwa tiketi ya Jubilee katika ikulu ya Nairobi.