Justin Muturi atoa wito kwa upinzani kuidhinisha viongozi wao bungeni

Spika wa bungeA� la taifa Justin Muturi ametoa wito kwa upinzani kudumisha mazoea ya awali katika kuidhinisha viongozi wao bungeni. Haya yanajiri malalamishi yaliyoibuliwa na mbunge waA� Lugari A�Ayub Savula kuhusiana na orodha ya wale walioteuliwa katika nyadhifa za uongozi katika bunge la taifa. Savula amesema chama cha A�ANC katika muungano wa NASA kimehadaiwa na kwamba spika anafaa kuingilia kati swala hilo. Mbunge wa Turkana Kusini A�James Lomenen ambaye anaegemea chama cha Jubilee amezua kichekesho aliposema kuwa spika anafaa kuingilia kati ili kuhakikisha kuwa upinzani unaidhinisha orodha ya viongozi wake bungeni. Wakati huo huo kiongozi wa wengi A�Aden Duale amemtaka spika kuachia viongozi wa upinzani kushughulikia mambo yao wenyewe. Hata hivyo spika A�Muturi ameahidi kuchunguza swala hilo kabla ya kutoa mwelekeo ili kuhakikisha shughuli za bunge hazitatiziki.