Justin Muturi apongezwa kwa kutupilia mbali rufaa iliyowasilishwa kotini

Baraza la kitaifa la mashirika yasiyo ya serikali limepongeza hatua ya bunge la kitaifa na spika wa bunge hilo, Justin Muturi ya kutupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na wakili mmoja wa Nairobi aliyekata utaraibu uzinduliwe kuwatimua jaji mkuu David Maraga, naibu wake, Philomena Mwilu pamoja na makamishna wengine watano wa tume ya kuajiri maafisa wa idara ya mahakama kwa madai ya utovu wa maadili. Kwenye taarifa mwenyekiti wa baraza hilo Stephen Cheboi amesema jaribio la kuwatimua jaji mkuu na wanachama wa JSC ke halikuwa na msingi wowote. Cheboi alisema jaribio lolote la kuvuruga uhuru wa idara ya mahakama lazima likataliwe mbali na wakenya. CheboiA� alitoa wito kwa wakenya kupuuza njama kama hizo na kuhakikishaA� wanaunga mkono uhuru wa asasi zote za umma kuambatana na katiba ya nchi hii. Hapo jana, Muturi alisema kwamba kujumuishwa kwa jaji mkuu kwenye rufaa hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa tume hiyo ya JSC na pia rais wa mahakama ya juu hakuwezi kuruhusiwa. Aliongeza kuwa mlalamishi huyo Adrian Njenga hakuzingatia utaratibu uliowekwa.