Justin Muturi akataa uteuzi wa John Mbadi

Spika wa bunge la taifa Justin Muturi amekatalia mbali uteuzi wa mbunge wa Suba kusini, John MBadi kuwa kiongozi wa walio wachache bungeni A�akisema A�uteuzi wake haukuzingatia utaratibu ufaao. Muturi alidokeza kwamba amepokea barua kutoka kwa vyama tanzu vya muungano wa NASA kuhusu suala hilo. Upinzani umeagizwa kuwasilisha orodha nyingine ya viongozi wake bungeni kufikia tarehe 17 mwezi Novemba. Kwenye mawasiliano spika wa bunge la taifa alisema amepokea barua nyingi kutoka vyama vya ODM, Ford-Kenya na ANC ambazo zinadai vyama hivyo vilikubaliana kuhusu nyadhifa fulani. Kanuni ya bunge nambari 20 sehemu ya 4 inaratibu kwamba ni kiranja wa walio wachache ambaye ana mamlaka ya kuwasiliana na spika kuhusu uongozi wa walio wachache bungeni. Mbadi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha ODM alisema muungano wa NASA hauna shida kuzingatia kanuni za bunge. Alisema muungano huo umekuwa ukifanya mashauriano kuhusu suala hilo katika bunge la taifaA� na lile la Seneti. Orodha iliyokataliwa ilimjumuisha John Mbadi kama kiongozi wa walio wachache na naibu wake Ayub Savula wa chama cha ANC. Robert Mbui ambaye ni mbunge wa Kathiani alitarajiwa kuwa kiranja wa walio wachache na naibu wake Chris Wamalwa wa chama cha Ford-Kenya.