Mbuge Junet Mohammed kufikishwa mahakamani

Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kukamatwa leo asubuhi kwa madai ya kutoa matamshi ya chuki. Inasemekana Junet alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Homa Bay ambako alihojiwa. Alikamatwa katika uwanja mdogo wa ndege wa Kabunde mjini Homa Bay kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi wiki mbili zilizopita kwenye kongamano la vijana lililohudhuriwa na naibu kiongozi wa chama cha ODM Ali Hassan Joho. Junet alikuwa miongoni mwa wabunge sita waliopewa lakabu ya a�?Pangani Sitaa�? ambao walikamatwa mwaka-2016 na kushtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki. Junet ni mkurugenzi wa uchaguzi katika chama cha ODM na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Jubilee.