Julius Malombe kuwasilisha rufaa dhidi ya Charity Ngilu

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Kitui, JuliusA�Malombe atawasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu uliodumisha kuchaguliwa kwa Charity Ngilu kuwa gavana wa kaunti hiyo. Kwenye ilani aliyotoa leo, Malombe alisisitiza kuwa Ngilu hakuchaguliwa kihalali kuwa gavana wa kaunti ya Kitui. Jaji wa mahakama kuu Pauline Nyamweya alidumisha uchaguzi wa Ngilu na kutupilia mbali rufaa ya Malombe akisema hakuthibitisha madai yake. Malombe alikuwa amepinga kuchaguliwa kwa Ngilu akisema ulikumbwa na dosari katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. Aidha alidai matokeo ya uchaguzi huo hayakuambatana na matakwa ya wapiga kura.