Juhudi za kuunda chama kimoja cha Amani National Congress kwa jamii ya waluyha imepuziliwa mbali

Juhudi za kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetangula za kuunda chama kimoja cha kisiasa kwa jamii ya waluhya zimepuuziliwa mbali na baadhi ya viongozi kutoka eneo la magharibi mwa nchi wanaounga mkono chama cha Jubilee. Kulingana na wabunge hao wakiongozwa na mbunge wa Sirisia JohnA� Walukhe, hatua ya viongozi hao wawili ni ya kujitakia makuu na wala sio msimamo wa jamii hiyo. Walukhe ambaye alichaguliwa kwa tiketi ya chama cha Jubilee alisema ni jambo lisilofaa kwaA� Wetangula na Mudavadi kubuni chama tofauti kwa Waluhya, wakati ambapo tayari kuna chama cha Jubilee ambacho kilishinda viti vingi katika eneo hilo na kuwateuwa watu kadhaa kutoka jamii hiyo katika nyadhifa za juu serikalini. Mwenzake wa mlima Kenya Fred Kapondi na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Trans Nzoia Janet Nangabo pia walitoa maoni sawa na hayo wakiwataka viongozi hao wawili sasa kuzingatia masuala yatakayostawisha jamii hiyo na waachane na siasa duni ziso na msingi.