Juhudi Za Kukabiliana Na Ugonjwa Wa Chikunguya Zaanza

Serikali imewaita maafisa wote wa matibabu waliopelekwa kusaidia kupambana na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika nchi za A�Sierra Leone na LiberiaA� kusaidia kukabiliana na kuzuka kwa ugonjwa wa Chikunguya humu nchini. Katibu katika wizara ya Afya Dr. Nicholas Muraguri amesema ingawa ugonjwa huo si hatari wizara ya afya imetoa tahadhari kwa madaktari katika kaunti za Mombasa, Lamu, Garissa na kaunti zilizopo katika eneo la mwambao wa pwani kuhusu kuzuka kwa ugonjwa huo. A�Thali hiyo imetokea huku serikali ikipeleka dawa za thamani ya shilingi milioni 80 kukabiliana na kuzuka kwa ugonjwa wa kipindu pindu na Chikunguya katika kaunti ya Mandera.