Juhudi Za Jaji Tunoi Kuendelea Kuhudumu Zagonga Mwamba

Jaji wa mahakama ya juu Philip Tunoi sasa atalazimika kunga��atuka wadhifa wake katika mahakama hiyo ya upeoni hapa nchini licha ya kesi ambayo amewasilisha mahakamani kupinga kustaafishwaA� baada ya kutimiza umri wa miaka 70. Tunoi alipoteza kesi aliyokuwa amewasilisha katika mahakama kuu lakini akaamua kwenda katika mahakama ya rufani kupinga uamuzi huo. Anadai kuwa hawezi kustaafu katika umri wa miaka 70 kulingana na katiba iliyorasimishwa mwaka 2010 kwani aliajiriwa wakati wa katiba ya zamani iliyotenga umri wa kustaafu kwa majaji kuwa miaka 74.Lakini tume ya huduma za mahakama inashikilia kuwa Tunoi aliajiriwa jaji wa mahakama ya juu chini ya katiba mpya na hivyo basi hana budi kustaafu kwa kutimiza umri wa miaka 70. Jaji huyo amehusishwa na madai ya ufisadi huku akishikilia kuwa anafaa kuendelea kuhudumu katika mahakama ya juu hadi atakapotimu umri wa miaka 74. Hapo jana Rais A�Uhuru Kenyatta alimsimamisha kazi Tunoi na kubuni jopo la kuchunguza madai ya ufisadi dhidi yake .Tunoi alikataa kujiuzulu kwa hiari akisema kuwa yuko tayari kujitetea mbele ya jopo litakalobuniwa kumchunguza.