Jubilee Yataka Raila Achunguzwe Na EACC

Viongozi wa mrengo wa Jubilee sasa wanamtaka kiongozi wa CORD, Raila Odinga kujibu madai kuhusu iwapo alidai pesa kutoka kwa msimamizi wa shamba la Dominion, Calvin Burgess. Wabunge hao wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la taifa, Aden Duale walisema tume ya maadili na kupambana na ufisadi inapaswa kuchunguza swala hilo na kutangaza hadharani wajibu wa Raila na gavana wa Siaya, Cornel Rasanga katika madai ya njama ya unyakuzi wa ardhi ambayo imekodishwa na mwekezaji huyo wa Marekani. Duale pia anataka tume hiyo ya kupambana na ufisadi, afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma na idara ya upelelezi hapa nchini kuanzisha uchunguzi kuhusiana na madai hayo. AlisemaA� Burgess anapaswa kutii maagizo ya kamati ya ardhi ya bunge la taifa ili kufafanua swala hilo.

Msimamizi wa makao makuu ya Jubilee, Raphael Tuju alisema uhasama dhidi ya wawekezaji umeathiri maendeleo katika eneo hilo huku watu wachache wakinufaika.A� Alipuuzilia mbali madai kwamba mrengo wa Jubilee ndio unahusika na madai ya Burgess, akisema hayawezi kupuuzwa.