Jubilee yapinga miito ya NASA ya kutimuliwa kwa maafisa wa IEBC

Mrengo wa chama cha Jubilee kwenye kampeni katika kaunti ya Nakuru, umepinga miito ya upinzani ya kutaka maafisa fulani wa tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC watimuliwe. Wanasiasa hao wa mrengo waA� Jubilee wakiongozwa na aliyekuwa mbunge wa Budalang`i, Ababu Namwamba walitoa wito kwa wakazi huko Nakuru wapuuze miito hiyo ya mrengo wa upinzani wa NASA. Ababu aliushutumu muungano huo wa upinzani unaoongozwa na Raila Odinga kwa kujaribu kuzua mzozo kwa kuendelea kushinikiza maandamano dhidi ya maafisa hao wa IEBC. Ababu aliwahimiza vinara wa muungano wa NASA Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetanga��ula kukubali kwamba IEBC ni tume huru. Aidha Ababu aliwahimiza wananchi kutoruhusu viongozi wabinafsi kuwatumia vijana kutimiza maslahi yao ya kisiasa.