Jubilee yamteua Davis Chirchir kuwa ajenti wake mkuu kwenye uchaguzi wa urais

Chama cha Jubilee kimemteua aliyekuwa waziri wa kawi Davis Chirchir kuwa ajenti wake mkuu kwenye uchaguzi wa urais. Chirchir atasaidiwa na Winny Guchu ambaye niA�A�mkurugenzi mkuu wa chama hicho. Naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe alidhibitisha uteuzi huo kwa shirika la utangazaji la KBC kupitia njia ya simu akisema tayari majina yao yamewasilishwa kwa tume ya IEBC. Uteuzi wao unajiri baada ya muungano waA�A�NASA kumteua seneta James Orengo kuwa ajenti wake mkuu katika uchaguzi wa urais akisaidiwa na afisa mkuu wa muungano huo Norman Magaya na majina yao kuwasilishwa kwa IEBC. Hatua hiyo ya Nasa na Jubilee ni sehemu muhimu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu na ule wa urais mnamo tarehe nane mwezi ujao. Vyama vinavyoshirika kwenye uchaguzi mkuu havijawateua maajenti wao katika maeneo bunge na vituo vya kura kuambatana na sheria.