Jubilee Yaidhinishwa katika eneo la Mlima Kenya mashariki

Viongozi katika eneo la Mlima Kenya mashariki wamekiidhinisha kwa kauli moja chama cha Jubilee ambacho wagombea watatumia kugomba nyadhifa tofauti tofauti katika uchaguzi mkuu ujao.

Akiongea na wandishi wa habari mwenyekiti wa chama hicho Noah Wekesa alisema tayari vyama saba vimejiunga na chama hicho na wanazungumza na vyama viwili viivyosalia ili kuhakikisha kuwa vinajiunga na chama hicho.

Kwa upande wake Seneta wa Meru, Kiraitu Murungi, ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa vyama hivyo alisema wanasubiri chama cha Jubilee kuimarika kwa sababu hawataruhusu chama kingine kujiunga na chama hicho baada ya kubuniwa rasmi.

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la seneti, Kithure Kindiki, alisema chama hicho kitaanda shughuli ya uteuzi kwa njia huru na ya haki na hakupaswi kuwa na hofu kwamba baadhi ya watu watapendelewa.