Jubilee yaahairisha uchaguzi wake wa mchujo Kaunti ya Nairobi

Chama cha Jubilee kimeahirisha uchaguzi wake wa mchujo kwenye Kaunti ya NairobiA� uliokuwa ufanyike leo hadi siku ya Jumatano tarehe 26 mwezi huu. Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju, alisema wameafikia uamuzi wa kuahirisha uchaguzi huo ili kuepusha hali ya kuingilia chaguzi za mchujo za chama cha upinzani-(ODM), ambazo zitaandaliwa Jumanne tarehe 25 April Jijini Nairobi. Tuju alisema kwamba chama cha Jubilee kiko tayari kuandaa uchaguzi wake wa mchujo lakini akahoji kwambaA� kaunti ya Nairobi ndiyo inatarajia ushindani mkali zaidi, ndiposa kuna haja ya kujipatia muda zaidi. Katika taarifa yake, Tuju alisema kwamba chama cha ODM tayari kimelipia vituo vingi vya kupigia kura, zikiwemo shule, na hivyo kuna haja ya kuahirisha tarehe za uchaguzi wa mchujo wa chama hicho.

Chama cha Jubilee kilitangaza tarehe mpya za kufanya chaguzi zake za mchujo siku ya Jumamosi tarehe 22 April, baada ya awamu ya kwanza ya zoezi hilo katika Jumla ya Kaunti 21 kutibuka siku ya Ijumaa tarehe 21 April. ChaguziA� hizo za mchujo sasa zitaanza siku ya Jumatatu kwenye kaunti za Baringo, Elgeyo Marakwet, Kirinyaga, Bomet na Nandi. Mnamo siku ya Jumanne, chaguzi hizo zitaandaliwa kwenye kauntiA� za Lamu, Wajir, Mandera, Marsabit, Turkana, Samburu, Kilifi, Tana River, Mombasa, Kitui, Machakos, Makueni, Bungoma, Busia, Homa Bay, Migori, na pia kwenye kaunti za Kwale, Garissa, Isiolo, Nyamira, Kajiado, Kiambu, Muranga na Uasin Gishu. Siku ya Jumatano chaguzi hizo zitaandaliwa kwenye Kaunti za Nairobi, Nyeri, Laikipia, Embu, Taita Taveta, Nyandarua, Narok, Nakuru, Meru, Tharaka Nithi, Pokot Magharibi na Trans Nzoia.