Jubilee wamepuzilia mbali pendekezo la Raila kuunda serikali ya muda

Viongozi kadhaa wa chama cha Jubilee wamepuzilia mbali pendekezo la kiongozi wa Muungano wa NASA Raila Odinga la kubuniwa kwa serikali ya muda ya kuongoza nchi hii kwa kipindi cha miezi sita ijayo.Wakiongozwa na mbunge maalum, Gideon Keter,viongozi hao walisema jubilee haina nafasi kwa mashauriano yoyote ya kugawana mamlaka. Waliushutumu upinzani kwa kwa kutokua aminifu kwenye matakwa yake wakisisitiza kwamba jubilee inaweza tu kushauriana na wakenya na wala sio mtu binafsi. Mbunge maalum, David Ole Sankok,aliye pia mwenyekiti wa baraza la kitaifa la walemavu alisisitiza kwamba pendekezo hilo halimo kwenye sheria.Kwenye mahojiano na shirika la habari la Roiters,Raila alisema yuko tayari kwa mashauriano na Rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na marekebisho ya katiba yanayonuiwa kupunguza uwezekano wa kuzuka kwa ghasia kutoka kwa makundi ya walio wachache yanayohisi kwamba yameachwa nje ya mamlaka.