Tuju Aidhinisha Uchaguzi Wa Mchujo Wa Jubilee

Mkuu wa makao makuu ya chama cha Jubilee Raphael Tuju, amethibitisha uadilifu wa uchaguzi wa mchujo wa chama hicho kama uliofanyika kwa njia huru bila mapendeleo. Tuju aliongeza kwamba tayari wamewachaguaA� maafisa wa muda wa chama hicho bila kuwahusisha wanaopania kuwania nyadhifa mbali mbali za uchaguzi kwa tikiti ya chama hicho. Akiongea wa mkutano uliowajumuisha maafisa wa chama hicho kutoka kaunti yaA� Kiambu huko Thika , Tuju alisema uteuzi wa wawaniaji wa Jubilee kwenye uchaguzi mkuu ujao utaandaliwa na tume huru ya uchaguzi nchini.Akikiri kwamba ukomavu katika maswala ya IEBC unahitajika upesi,Tuju alimtaka kinara wa Cord Raila Odinga kutojihusisha na maswala ya tumeA� hiyo yaA� IEBC.

Wakati uo huo, Migawanyiko iliyotokana na uchaguzi wa maafisa wa chama cha Jubilee uliokumbwa na utata katika kaunty ya Nakuru ungalipo huku walioshindwa kwenye uteuzi huo wakisema watabuni afisi sambamba ya kusimamia kampeini za chama hicho. Mwanasiasa mmoja wa Naivasha , James Karimi, aliyeshindwa na David Manyara kwenye kinyanganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti amekuwa akikutana na wanachama mbali-mbali wa chama hicho kutoka wadi 55 za kaunty hiyo kwa lengo la kubuni kundi sambamba la kukifanyia kampeini chama cha Jubilee.