Jopo Linalochunguza Jaji Tunoi Kufanya Vikao Vyake Hadharani

Jopo linalochunguza mienendo ya jaji wa mahakama ya juu aliyesimamishwa kazi Philip Tunoi linasema vikao vyake vitafanyika hadharani. Kwenye taarifa kwa wana-habari Jopo hilo lilisema Justice Tunoi amebadili kauli yake na kutaka vikao hivyo kufanyika hadharani kinyume cha ombi lake la awali kwamba vifanyike kwa faragha. Jopo hilo lilianza vikao vyake siku ya Jumanne A�, huku shahidi mkuu Geoffrey Kiplagat akifika mbele yake. Jopo hilo lilibuniwa na Rais Uhuru Kenyatta, kubaini iwapo Justice Tunoi anafaa kuendelea kuhudumu, kufuatia madai ya mwana-habari Geoffrey Kiplagat kwamba alihongwa zaidi ya shilingi milioni- 200A� na gavana wa Kaunti ya Nairobi Dr. Evans Kidero kwenye kesi ya kupinga uchaguzi wake ambayoA� iliwasilishwa na mbunge wa Kabete Ferdinand Waititu.