Jopo la Ukufunzi ya Timu Ya Sony Sugar Yakamilika

Jopo la ukufunzi la timu ya soka ya Sony Sugar sasa limekamilika baada ya kunga��atuka kwa naibu wa kocha Salim Babu; meneja wa timu Stoke Ouma, na mshauri wa walindalango Gaddy Kawuondo kujazwa na kocha mkuu Leonard Odipo, kulingana na jukumu alilopewa na uongozi wa kilabu hicho.

Timu ya Sony Sugar ilianza kusuasua katika michuano ya ligi msimu huu hususan baada ya kucheza mechi tano bila ushindi, matokeo yaliyochangiaA� kutimuliwa kwa maafisa hao.

Aliyekuwa mkufunzi wa Mathare United Collins Omondi ameteuliwa kuwa naibu wa kocha na kukabidhiwa jukumu zaidi laA� kuwashauri walindalango naye aliyekuwa mlinzi katika timu hiyoA� Emmanuel Geno akiteuliwa kuwa meneja wa kikosi.

Mlinzi wa muda mrefu Sylvester Wanyama, amepandishwa wadhifa na sasa atakuwa kocha mchezaji tikio lotakalomwezesha kuwa naibu wa kocha mwezi wa Juni mwaka huu. Kufuatia uteuzi huo, sasa kiungo Victor Ayugi atakuwa nahodha wa timu akisaidiwa na Kevin Oluoch na Nicholas Akoko.