Joho hatimaye aongea kuhusu madai ya kugushi cheti chake cha KCSE

Gavana wa Mombasa Hassan Joho hatimaye amevunja kimya chake kuhusu madai ya yeye kugushi cheti cha matokeo ya mtihani wake wa kidato cha nne mwaka wa 1992. Joho anasema alifanya mtihani wa kidato cha nne mwaka wa 1993 na kupata alama ya D- kinyume cha madai ya ugushi kwamba aliweza kupata alama ya C+ kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka wa 1992. Gavana huyo ameilaumu serikali ya Jubilee kwa masaibu yake, akisema kwamba hatakubali kuyumbishwa na hila za serikali za kumtaka anga��atuke kutoka uchaguzi wa mwezi Agosti. Masaibu yake yanadaiwa kuanza wakati barua iliyoandikiwa mkurugenzi wa upelelezi Ndegwa Muhoro kutoka kwa baraza la taifa la mitihani KNEC ilisema kwamba walishindwa kubainisha uhalali wa hati ya matokeo ya mtihani wake wa kidato cha nne mwaka wa 1992 kama ilivyowasilishwa na gavana huyo. Kulingana na baraza la KNEC, jina la gavana Joho na nambari yake ya usajili kwa mitihani hazina kwenye sajili ya bodi hiyo na huenda alighushi vyeti hivyo. Gavana huyo anadai masaibu yake yalianza mwaka wa 2013 wakati mtu asiyejulikana alikamatwa na polisi katika sehemu ya burudani jijini Nairobi, akibadili na kugushi hati zake za msomo ili kumfedhehesha, njama ambayo anadai ilipangwa na wapinzani wake.Joho hata hivyo hajapuuzilia mbali cheti hicho cha mwaka 1992 na amekataa kutoa maoni kuhusu suala linalozua utata kuhusu jinsi alivyojiunga na chuo kikuu cha Nairobi. Joho leo anatarajiwa kuandikisha taarifa katika makao makuu ya kanda ya mkurugenzi wa idara ya upepelezi huko Mombasa kubainisha uhalali wa cheti chake cha masomo