Joho Akataa Maafisa Wa Usalama Waliotumwa Kumlinda

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amedai kwamba alikatalia mbali maafisa wa usalama waliotumwa kumlinda baada ya kufahamu kwamba maafisa hao wangelitumiwa kuweka ushahidi bandia nyumbani kwake ili utumike kumfungulia mashtaka.Ilikuwa mara ya kwanza kwa Joho kuzungumzia swala hilo baada ya uamuzi wake wa kukataa ulinzi wa maafisa wa usalama.

Joho aliyekuwa akiongea wakati wa hafla ya kuwahamasisha watu kujisajili kama wapiga kura katika ukumbi wa Treasury mjini Mombasa,alisema kuwa anajihisi yuko salama bila walinzi wa serikali.Gavana huyo aliyekuwa ameandamana na baadhi ya wabunge wa upinzani kutoka Mombasa alitoa wito kwa wakazi kujisajili kwa wingi kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu.