Johnstone Muthama Afika Mbele Ya Tume Ya Kitaifa Ya Mshikamano Na Utangamano Kujibu Madai Ya Kutoa Matamshi Ya Chuki

Seneta wa Machakos Johnstone Muthama alifika mbele ya tume ya kitaifa ya mshikamano na utangamano kujibu madai ya kutoa matamshi ya chuki alipokuwa katika kaunti ya Busia hivi majuzi. Mnamo Jumatatu, Muthama alikataa kuandikisha taarifa kwa polisi au kuhojiwa na maafisa wa usalama akisisitiza kuwa madai dhidi yake ni uwongo. Tume hiyo chini inayoongozw ana Francis Ole Kaparo ilimwagiza Muthama kufika mbele yake kufafanua zaidi kuhusu madai hayo. Muthama anakabiliwa na shutuma za kueneza chuki kwa kutoa matamshi yasiofaa kwenye mkutano wa mrengo wa CORD, kaunti ya Busia wakati wa hafla ya kumkaribisha mwakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo Florence Mutua aliyekamatwa na kuzuiliwa korokoroni kwa siku nne kwa madai ya kueneza chuki.