Zimbabwe ingali katika hali tatanishi

Raia wa Zimbabwe wanasubiri kuona hatua wanajeshi watachukua baada ya kutwaa uongozi wa nchi hiyo. Rais wa nchi hiyo A�Robert Mugabe anasemekana kuzuiliwa nyumbani kwake mjini Harare, lakini habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa mkewe Grace, aliyekuwa ametangaza azma ya kumrithi ametorokea nchini Nambia. Jeshi lilichukua hatua hiyo kufwatia kufutwa kazi kwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa, ambaye mpinzani mkubwa wa mkewe Bi. Grace Mugabe.Mahali aliko A�Mnangagwa pia hapajulikani. Mugabe aliye na umri wa miaka 93, ameitawala nchi hiyo tangu ilipopata kutoka kwa Uingereza mnamo mwaka 1980. Mzozo kuhusu anayepasa kumrithi Mugabe, kati ya Grace na Mnangagwa umekigwanya chama tawala cha Zanu-PF katika miezi ya hivi majuzi..