Jeshi La Uturuki Latwa Mji Wa Jarablus

Latest Video on Turkey Army Attacks on Syriaa��s Jarablus

Jeshi la Uturuki na washirika wake limepenyeza zaidi nchini Syria na kutwaa eneo lililomilikiwa na vikosi vinavyoungwa mkono na Wakurdi katika siku ya tano ya makabiliano mpakani ambayo kundi linalokadiria hali nchini humo limesema yamesababisha vifo vya wanakijiji 35. Uturuki ilisema wanamgambo 25 wa Kikurdi waliuawa kwenye mashambulizi yake ya angani na kukanusha madai kwamba kulikuwa na raia waliouawa. Hakukuwa taarifa iliyotolewa mara moja na kundi la YPG, lakini vikosi ambavyo ni washirika ya kundi hilo vimesema kundi hilo lilikuwa limeondoka eneo hilo kabla ya shambulizi hilo kutekelezwa.

Uturuki ambayo pia inakabiliana na waasi wa Kikurdi nyumbani, ilipeleka vifaru na wanajeshi nchini Syria siku ya Jumatano kuwasaidia washirika wake waasi nchini Syria. Vikosi hivyo vinavyoungwa mkono na Uturuki kwanza vilitwaa mji wa mpakani nchini Syria wa Jarablus kutoka kwa wanamgambo wa kundi la Islamic State kabla ya kuelekea kusini katika maeneo yanayokaliwa na wanamgambo wa Kikurdi. Maafisa wa Uturuki wanasema lengo lao nchini Syria ni kuhakikisha vikosi vya kikurdi havitwai maeneo zaidi kwenye mpaka wa Uturuki na pia kuliondoa kundi la Islamic State kutoka kwa ngome zake.