Jeshi la Uganda lathibitisha kuua wanajeshi watatu wa Somalia

Jeshi la Uganda lathibitisha kuua wanajeshi watatu A�wa SomaliaJeshi la Uganda limethibitisha kuwa liliwaua wanajeshi watatu wa Somalia mwishoni mwa wiki. Jeshi hilo limeshutumu wanajeshi wa Somalia kwa kufyatulia risasi msafara wa kamanda wa kikosi cha wahifadhi amani nchini humo ndiposa likajibu shambulizi hilo. Msemaji wa jeshi hilo la Uganda, Bigedia Richard Karemire aliliambia shirika la habari la Roita kuwa wanajesho hao walizuiliwa katika kituo kimoja cha barabarani walipokuwa wakielekea kambini baada ya kutoa huduma za matibabu kwa watu waliojeruhiwa kwenye shambulizi la bomu lililosababisha vifo vya watu-38 mnamo jumamosi. Aliongeza kuwa uchunguzi unaendelea lakini kanuni za kikosi cha AMISOM zinaruhusu wanajeshi kujibu shambulizi wanapolengwa. Hata hivyo, afisa mmoja wa usalama nchini Somalia, Mohamed Ali alilaumu kikosi cha AMISOM kwa shambulio hilo akisema wanajeshi wa Somalia walikuwa na haki ya kusimamisha msafara huo baada ya kutangazwa kwa tahadhari mjini humo.