Jeff Sessions aidhinishwa kuwa mkuu wa sheria Marekani

Bunge la seneti nchini Marekani limeidhinisha uteuzi wa seneta Jeff Sessions kuwa mkuu wa sheria wa nchi hiyo licha ya kuibuka kwa mjadala mkali kuhusu rekodi yake ya ukiukaji haki za binadamu na juhudi za maseneta wa chama cha Democratic za kuzuia uteuzi wake. Sessions aliyependekezwa na rais Donald Trump aliidhinishwa kwa kuraA�A�52 dhidi ya 47. Sessions alikuwa anakabiliwa na madai ya ubaguzi wa rangi na anachukua wadhifa huo huku maafisa wa kitengo hicho wakitetea vikali marufuku ya muda iliyotangazwa na rais Trump dhidi ya raia wa mataifa saba ya Kiislamu. Mahakama ya rufani nchini Marekani inatarajiwa kutoa kauli yake juma hili kuhusu marufuku hiyo.