Jassi Chatthe Ashinda Makala Ya 64 Ya Mashindano Ya Magari Ya Safari Rally

Bingwa mtetezi Jassi Chatthe ndiye tena bingwa wa makala ya 64 ya mashindano ya magari ya Safari Rally baada ya kushinda katika siku ya mwisho ya mashindano hayo hapo jana. Chatthe alishinda mashindano hayo mbele ya Rajbir Rai na Tapio Laukkanen waliomaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia. Licha ya kushinda mashindano hayo Chatthe anashikilia nafasi ya pili kwenye orodha ya kitaifa ya mashindano ya magari kwa alama 57.5 nyuma ya Rajbir Rai anayeongoza kwa alama 60.5. Tapio Laukkanen ni wa tatu kwa alama 56.

Ramesh Vishram alishinda kitengo cha a�?Classica�� naye Asad Khan akaibuka mshindi wa kiwango cha a�?SPVa�� mbele ya Adil Mirza na Geoff Mayes waliomaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia. Alex Lairangi alishinda kitengo cha magari yanayovutwa kwa magurudumu mawili baada ya kumpiku Leonardo Varese huku Ian Duncan, Carl Tundo na Farhaaz Khan wakishikilia nafasi tatu za mwanzo kwenye kitengo cha a�?Na�� mtawalia.A�