Korea Kaskazini Yatekeleza Jaribio La Kombora La Nyuklia

 

A�Korea Kaskazini imesema imetekeleza jaribio la kombora la kinuklia kukabiliana na kile ilichosema uhasama wa Marekani dhidi ya taifa hilo. Tetemeko la ardhi la kiwango cha-5.3 kwenye mizani ya ritcher lilitokea leo asubuhi katika kile shirika la kukadiria mitetemeko ya ardhi nchini Korea Kusini lilitaja kuwa mlipuko mkubwa kuwahi kutokea. Tetemeko hilo lilitokea karibu na mahali ambapo jaribio la kombora hilo la kinuklia lilitokea. Mnamo mwezi Januari mwaka huu, Korea Kaskazini ilitekeleza jaribio la nne la kombora lake la kinuklia katika eneo hilo hilo. Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye alitaja hatua hiyo kuwa ukiukaji mkubwa wa maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Naye rais Baraka Obama wa Marekani alisema hatua hiyo ya Korea Kaskazini itavutia adhabu kali huku akikariri kuwa Marekani imejitolea kuhakikisha usalama wa washirika wake katika bara la Asia na ulimwengu mzima. Msemaji wa serikali ya Japan alisema nchi hiyo itakadiria kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo zaidi.