Jamii Ya Wamaasai Kujitenga Na Jubillee Kwa Uchaguzi Ujao

Baadhi ya viongozi wa Ki-siasa kutoka jamii ya Wa-Masaai wametishia kuacha kukiunga mkono chama cha Jubilee wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Wakiongozwa na Seneta wa Kaunti ya Narok Stephen Ole Ntutu wabunge hao walidai utawala wa Jubilee haujatimiza ahadi zake kwa jamii ya wa-Maasai. Hayo yanajiri huku Naibu Rais William Ruto akiimarisha kampeini za kukipigia debe chama hicho mpya, kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Kwingineko seneta wa Kaunti ya Nyamira Okonga��o Monga��are amepuuzilia mbali barua iliyotiwa saini na kiranja wa walio wachache katika bunge la seneti Johnston Muthama kutafuta kufutilia mbali kwa uteuzi wake katika kamati ya bunge juu ya uhasibu wa fedha za Umma. Monga��are aliyechaguliwa mahala pa Dr. Bonny Khalwale amesisitiza kwamba alichaguliwa ki-halali kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya uhasibu wa fedha za umma.