Jaji Mkuu Willy Mutunga Aahirisha Hadi Tarehe 2 Juni Kusikilizwa Kwa Rufaa Iliyowasilishwa Katika Mahakama Ya Juu Na Naibu Jaji Rawal Na Tunoi

Jaji mkuu A�Willy Mutunga ameahirisha hadi tarehe mbili Juni siku iliyowekwa na jaji Njoki Ndunga��u ya kusikilizwa kwa rufaa iliyowasilishwa katika mahakama ya juu na naibu jaji mkuu Kalpana Rawal na jaji Philip Tunoi ya kupinga kustaafu kwao katika umri wa miaka A�70. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari A�Mutunga amesema jaji A�Njoki Ndunga��u alitoa maagizo hayo kwenye rufaa iliyohitaji A�kuidhinishwa kuwa ya dharura . Amesema ametumia mamlaka yake kama jaji mkuu na rais wa mahakama ya juu kuharakisha vikao vya kusikilizwa kwa rufaa hiyo. Amemwagiza msajili wa mahakama ya juu kuagiza pande zote kuhudhuria vikao vya kusikiliza pande zote kwenye kesi hiyo mbele ya jopo la majaji watano wa mahakama ya juu ambao ni pamoja na yeye, majaji A�Ndung’u, Smokin Wanjala, Mohammed Ibrahim na A�Jackton Ojwang’ mnamo tarehe mbili Juni mwaka huu kuanzia saa nne asubuhi.m