Jaji Mkuu Willy Mtunga Leo Atarajiwa Kutoa Hotuba Yake Ya Mwisho katika Bunge La Senate

Jaji mkuu Willy Mutunga leo anatarajiwa kutoa hotuba yake ya mwisho katika bunge la Senate kabla ya kustaafu hapo kesho. Mutunga ambaye pia ni rais wa mahakama ya juu atastaafu mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa kipindi chake mwezi Juni mwaka ujao. Mutunga aliteuliwa mwezi Juni mwaka 2011 na ametekeleza marekebisho kadhaa katika idara ya mahakama. Katika kipindi cha kuhudumu kwake aliongoza kusikizwa kwa rufaa iliyohusu matokeo ya uchaguzi wa urais iliyowasilishwa na Raila Odinga ambayo ilikuwa ya kwanza chini ya katiba mpya. Wakati huo Odinga alikuwa amepinga kuchaguliwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa rais.