Jaji Mkuu Aandaa Baraza La Kitaifa La Utekelezaji Haki

Jaji mkuu Dkt. Willy Mutunga leo ataanda mkutano wa baraza la kitaifa la utekelezaji haki kujadili miongoni mwa masuala mengine , ushirikiano miongoni mwa taasisi mbali mbali katika kukabiliana na ufisadi pamoja na masuala kuhusu utekelezaji haki kwa kuzingatia mfumo wa ugatuzi. Mkutano huo utapokea ripoti kutoka taasisi zote za kupambana na ufisadi na kukubaliana kuhusu mikakati ya pamoja na kukabiliana na zimwi hilo. Msajili mkuu wa idara ya mahakama Ann Amadi amesema tume ya kupambana na ufisadi imealikwa kutoa mawasilisho yake kwenye mkutano huo. Mkutano huo pia utajadili miakati makhsusi miongoni mwa taasisi za kupambana na ufisadi na baraza la magavana. Haya yanajiri huku juhudi zikiimarishwa serikalini kukabiliana na ufisadi.