Jaji David Maraga Ateuliwa Kuwa Jaji Mkuu Wa Kenya

Jaji David Maraga ameteuliwa kuwa jaji mkuu mpya wa Kenya. Mwenyekiti wa tume ya kuajiri wahudumu wa idara ya mahakama Profesa Margaret Kobia alisema jina la Maraga sasa litawasilishwa kwa rais Uhuru Kenyatta hapo kesho uteuzi rasmi. Endapo ataidhinishwa na rais, Maraga mwenye umri wa miaka 65 atachukua mahali pa jaji Dr Willy Mutunga aliyestaafu mwezi Juni mwaka huu. Maraga ambaye alihudumu huko Kisumu kama jaji wa mahakama ya rufaa alikuwa wa tatu miongoni mwa wawaniaji 11 waliohojiwa na jopo la uteuzi la tume ya kuajiri wahudumu wa mahakama kwa wadhifa wa jaji mkuu.