Jackson Ole Sapit Aapishwa Kuwa Askofu Mkuu

Aliyekuwa askofu dayosisi ya Kericho ya kanisla la Kiangilikana, Jackson Ole Sapit, ameapishwa kuwa askofu mkuu wa kanisa hilo hapa nchini na pia askofu wa dayosisi ya All Saintsa�� Cathedral. Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi mashuhuri waliohudhuria sherehe hiyo. Ole Sapit, aliye na umri wa miaka 52 alibatizwa mwaka 1977. Wajibu wake wa kwanza ulikuwa kuhubiri injili na uhamasishaji jamii huko Narok, wajibu ambao aliutekeleza kwa miaka miwili, kabla ya kujiunga na taasisi ya theolojia ya Berea huko Nakuru. Alitawazwa kuwa shemasiA� mwezi Julai mwaka 1991, na kisha kuwa kasisi mwaka mmoja baadaye.